Breaking

Jumamosi, 11 Oktoba 2025

TUWAJIBU WAPOTOSHAJI KWENYE SANDUKU LA KURA.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewataka wanawake wa Wilaya ya Tanganyika kujibu upotoshaji  wa mitandao unaotaka kuvuruga amani na Mshikamano wa Nchi,  kwa kujitokeza kwa wingi na kupiga kura ifikapo oktoba 29.

Akizungumza baada ya kuwasili wilaya Tanganyika tarehe 10 Oktoba 2025, ikiwa ni muendelezo wa kampeni Chatanda, amesema watu hao hawapaswi kujibiwa kwa maneno bali kwa kuipa ushindi CCM na kushika Dola






Katika mkutano huo Chatanda alimuombea kura za ndiyo Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja, kumnadi mgombea wa Ubunge  jimbo la Tanganyika, Moshi Selemani Kakoso, na Wagombea Udiwani kwa tiketi ya CCM, ndani ya Jimbo hilo.

Hakuna maoni: