Breaking

Ijumaa, 10 Oktoba 2025

SERIKALI YADHAMIRIA KUJENGA TANZANIA YA KIDIJITALI KUPITIA TEHAMA

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nicholas Mkapa amesema serikali inaendelea kusimamia eneo la Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)kuhakikisha Tanzania ya kidigitali inakua halisi na kuakisiwa na sekta zote ikiwemo Posta.

Mkapa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam Wakati  akizungumza na wadau mbalimbali walioudhuria Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani yakiwa na Kauli Mbiu isemayo “Posta kwaajili ya watu, Huduma za Kizawa. Ufikaji Kimataifa”

Ameeleza kuwa, lengo la kufanya mageuzi hayo ya Teknolojia katika ulimwengu wa digitali, ni kuendeleza uwezo wa wananchi hususan vijana kupata usuluhishi wa changamoto zinazokabili Taifa na kujenga kizazi kipya chenye dira, ujasiri na uwezo wa kubadili mustakabali wa Tanzania kuwa Taifa la kidijitali na kibiashara.

Akimwakilisha Postamasta Mkuu Macrice Mbodo, Mkurugenzi wa Huduma za posta, Arubee Ngaruka amesema shirika hilo limeendelea kuongeza ubunifu wa kidigitali  kuendana na mageuzi yaliyopo sasa katika teknolojia.

Amesema katika kutekeleza hilo, wamefanikiwa kuanzisha mfumo wa biashara mtandaonio ambapo unafikiwa na wadau wote wa nchi wanachama wa Posta duniani, jambo ambalo ni fursa kwa wafanyabiashara nchini kujiunga.

Hakuna maoni: