Breaking

Jumanne, 28 Oktoba 2025

πŸ’– SIMULIZI: MWANGA WA USIKU

Sehemu ya Pili



Siku iliyofuata nilijikuta nikitembea tena barabarani pale pale, moyo wangu ukitamani kumuona Neema.

Lakini safari hii, benchi lile lilikuwa tupu  kama vile upepo ulikuwa umechukua kumbukumbu ya usiku ule.

Nilihisi pengo lisiloelezeka.

Nilitaka kumuona, sio kwa sababu ya maneno tuliyozungumza, bali kwa utulivu aliounyesha katikati ya maumivu aliyoyataja bila kuyaeleza.

Siku zikapita, wiki zikapita.

Kila nilipopita pale nilitamani kuona tabasamu lile lile lililokuwa na siri.

Hatamaye mwezi sasa umepita pila kumuona Mrembo Neema, sikuchoka lakini πŸ˜ƒ

Ila siku moja wakati nakatiza tena eneo lile, nilimuona tena.

Alikuwa amevaa gauni jeupe, akiwa amekaa kwenye bustani. Mikononi mwake ameshika maua, nikamsogelea kwa furaha kubwa.

“Nimefurahi kukuona tena,” nilisema kwa tabasamu lisilofichika.

“Na mimi pia,” alijibu kwa sauti ya utulivu. “Nilihitaji mtu wa kuongea naye, ila sikuwa najua kama ulimwengu utanirudishia wewe.”

Tulikaa tukizungumza kwa muda mrefu.

Kila neno lake lilikuwa na uzito  kama lililopitia maumivu mengi kabla ya kutoka midomoni.

Niligundua alikuwa amepoteza mama yake miezi mitatu iliyopita, na maisha yake yamekuwa magumu tangu siku hiyo.

“Lakini,” alisema akinitazama machoni, “nimejifunza kitu… wakati mwingine mwanga unaokuongoza hauji kutoka juu, bali kutoka kwa mtu anayekaa karibu yako kimya.”

Maneno hayo yalinikaa kichwani.

Siku hiyo nikajua  Neema hakutokea tu kama bahati, bali kama somo la maisha. πŸŒ™


πŸ’‘ Somo la Sehemu ya Pili:

Wakati mwingine Mungu hututumia watu kama taa za muda, ili kutuonyesha njia tunapopotea gizani.


Haya jamani Neema na Nelson wameonana tena kwa mara ya pili na wamezungumza ila kunaonekana kuna kitu hakiko sawa kwa Neema ni kitu gani hicho???

πŸ—“️ Endelea na Sehemu ya Tatu hapa KONA YA SIMULIZI  ndani ya Madelemo News.

Hakuna maoni: