Manchester City na Real Madrid wanamfuatilia winga wa Ufaransa Michael Olise huku Bayern Munich wakifikiria kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mkataba ulioboreshwa. (Team Talks)
Tottenham wanatazamiwa kukubaliana kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Uruguay Rodrigo Bentancur, 28, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika msimu wa joto wa 2026. (Athletic - Subscription Required)
Arsenal wako tayari kumlipa mshambuliaji wa Uingereza Bukayo Saka, 24, ambaye kandarasi yake inakamilika msimu wa joto wa 2027, zaidi ya pauni 250,000 kwa wiki. (Sportsport)
Southampton wanapanga kumpa kiungo wa kati wa West Ham Muingereza James Ward-Prowse, 30, nafasi ya kurejea St Mary's mwezi Januari. (GiveMesport)
Bayern Munich inanuia kumbakisha kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na Senegal Nicolas Jackson, 24, kwa msingi wa kudumu hata kama masharti ya wajibu wa kumnunua kwenye mkataba wake hayatatimizwa. (TBR Football)
#ChanzoBbcswahili


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni