Breaking

Jumatatu, 13 Oktoba 2025

WAZIRI MWIGULU AUNGA MKONO KAMPENI YA KUKATAA JEZI FEKI, ANUNUA JEZI 200 ORIJINO

 

Waziri wa Fedha na mdau wa michezo nchini, Dkt. Mwigulu Nchemba ameunga mkono kampeni ya kuhamasisha mashabiki kukataa jezi feki na kununua orijino kwa kununua jezi 200.

Licha ya kununua jezi hizo lakini pia Dkt. Nchemba amewataka mashabiki kununua bidhaa za klabu kwani kwa kufanya hivyo wanasaidia kuinua uwezo wa kifedha wa klabu jambo ambalo linaisaidia taasisi kujiendesha kikamilifu.

Pia Dkt. Nchemba amepongeza ziara ambayo tunaendelea kuifanya ya kutoa elimu kwa mashabiki wetu na kuzishauri taasisi nyingine kujifunza kwa Simba namna ambavyo tunawafuata mashabiki wetu katika maeneo yao ili kuwapa elimu.

Hakuna maoni: