Breaking

Jumatatu, 13 Oktoba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU: BARCELONA YAGOMA KUMUONGEZEa MKATABA ROBERT LEWANDOWSKI

 

Barcelona haitamuongezea mkataba mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 37, mkataba wake utakapokamilika msimu ujao. (Sport - In Spanish)

Barcelona wako tayari kuchukua chaguo la kufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji Marcus Rashford, 27 kutoka Manchester United kuwa wa kudumu kufuatia kiwango kizuri cha mchezo wake mapema msimu huu. (Sun)

Kipa wa England Jordan Pickford, 31 anatazamiwa kuongeza muda wake wa kuitumikia Everton kwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na The Toffees. (Times Subscription Required}


Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane anapanga kurejea kwenye uongozi na angependa kuinoa timu ya Ufaransa. (Mirror)


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: