Breaking

Alhamisi, 13 Novemba 2025

RAIS SAMIA AMTEUA DKT. MWIGULU NCHEMBA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.


Jina la Dkt. Mwigulu limewasilishwa leo Alhamisi, Novemba 13, 2025, bungeni na mpambe wa Rais kwa Spika wa Bunge, Mussa Zungu, kabla ya kusomwa kwa wabunge ili kuthibitishwa kwa kura.


Dkt. Mwigulu, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida, atachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Kassim Majaliwa, aliyelitumikia taifa katika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 2015 hadi 2025.


Hakuna maoni: