Breaking

Jumatano, 19 Novemba 2025

SIMBA SC YAITHIBITISHA CAMARA AFANYIWA UPASUAJI MOROCCO



Golikipa wa Simba Sports Club, Moussa “Pinpin” Camara, amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Morocco baada ya kupata jeraha lililomweka nje ya dimba kwa muda.


Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, Camara anatarajiwa kukaa nje kwa takribani wiki 8 hadi 10 ili kupatiwa matibabu na kuendelea na hatua za urekebishaji kabla ya kurejea uwanjani.


Simba SC imetoa shukrani kwa wataalamu wa tiba nchini Morocco na kuwataka mashabiki kuendelea kumuombea golikipa huyo aweze kurejea akiwa na afya njema.


Hakuna maoni: