Breaking

Jumatano, 19 Novemba 2025

ENDELEZENI UHUSIANO NA WALIPAKODI - CG MWENDA

 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amewataka watumishi wa TRA  kuendeleza uhusiano mzuri na walipakodi kwa kuwahudumia kwa weledi na kwa kuzingatia sheria.

Ameyasema hayo tarehe 18.11.2025 alipotembelea ofisi za TRA Dodoma na kuzungumza na watumishi akiambatana Menejimenti ya TRA.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema uhusiano mzuri baina ya TRA na walipakodi siyo tu unajenga imani ya walipakodi kwa mamlaka, bali pia unachochea ulipaji wa kodi kwa hiari na kuongeza mapato ya serikali kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

"Endeleeni kuimarisha uhusiano na Walipakodi kwa kuwatembelea kuwasikiliza na kutatua changamoto zao kwa wakati, hilo litaendelea kujenga imani ya walipakodi waliyonayo kwetu" amesema Bw.  Mwenda.

Aidha, alitoa pongezi kwa watumishi wa TRA Dodoma kwa jitihada zao katika kutekeleza majukumu ya ukusanyaji mapato na kuwataka waendelee kubuni mbinu bora zaidi zitakazosaidia kuongeza wigo wa walipakodi huku wakidumisha maadili ya kazi.

Katika hatua nyingine Kamishna Mkuu Mwenda ameeleza kuridhishwa na jengo jipya la ofisi za TRA mkoa wa Dodoma ambalo litaboresha zaidi huduma za kodi kwa kuwahudumia walipakodi katika mazingira mazuri na rafiki.

Hakuna maoni: