Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Utali Tanzania (TCT) na Mtendaji Mkuu wa Wamiliki wa Hotel Tanzania (HAT) Bi. Lathifa Sykes ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa karibu na wadau wa utalii akitoa rai kwa TRA kuendelea kuboresha mazingira ya ulipaji kodi katika sekta ya utalii ili kuimarisha hamasa iliyopo ya ulipaji kodi wa hiari.
Bi. Lathifa ameyasema hayo tarehe 17.11.2025 jijini Arusha alipokutana na Meneja wa TRA wa Mkoa huo, Bw. Deogratius Shuma kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya kodi.
Aidha, kikao hicho kilihudhuriwa na wadau wengine wa sekta hiyo pamoja na watumishi wa TRA wa mkoa wa Arusha





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni