Breaking

Jumatano, 10 Desemba 2025

MEZA YA MAGAZETI LEO – DESEMBA 10, 2025

 


Karibu kwenye Meza ya Magazeti ya Jumatano, Desemba 10, 2025, ambapo tunakuletea kwa ufupi na kwa uthabiti habari kubwa zilizobebwa kwenye kurasa za mbele za magazeti nchini. Hizi ndizo taarifa zinazotawala leo katika siasa, uchumi, jamii na michezo.


MWANA SPOTI


Gazeti la MwanaSpoti leo limeibeba headline kubwa: “KOCHA MPYA KUAMUA”, likiibua mjadala kuhusu mabadiliko ndani ya klabu moja kongwe nchini.


Mengine yaliyomo ndani ya gazeti hilo:


  • Kipigo cha Azam FC Chamg’anda Matola – matokeo yasiyoridhisha yakitajwa kuongeza presha kwa benchi la ufundi.
  • Mreno Amuamusha Mousa Balla Conte – taarifa za kuongezeka kwa ubora wa straika huyo.
  • Pacome, Doumbia Wapewa Siku Saba – majukumu ya ndani ya klabu yakizidi kuwabana mastaa hawa.
  • Simulizi ya Ndemla Yenye Utamu na Maumivu – maisha na safari ya kiungo huyo kwenye soka la ushindani.
  • Mechi za leo Ulaya: Madrid v City, Brugge v Arsenal, Bilbao v PSG.



ZANZIBAR LEO


Gazeti la Zanzibar Leo limeibuka na habari kuu:



“Rais Samia Asamehe Wafungwa 1,036”



Katika maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika, baadhi ya wafungwa wamepunguziwa adhabu huku wengine wakiachiwa huru moja kwa moja.


Habari nyingine:


  • Bei ya Mafuta Yashuka – pengo la bei ya dizeli na petroli lapungua, likileta nafuu kwa wananchi.
  • Serikali Kutumia Dola 400M Kufukia Bahari – hatua ya kimkakati katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
  • Chuo cha Uvuvi Kujengwa Shumba Mjini – mradi unaotarajiwa kuongeza ujuzi na ajira katika sekta ya uvuvi.
  • Hali Ni Shuwari – DCP Msimbe – ufafanuzi wa Jeshi la Polisi kuhusu usalama wa wananchi.















Hakuna maoni: