Breaking

Jumatano, 16 Julai 2025

SIMBA HAITAZUILIKA MSIMU UJAO-MO DEWJI

 

Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji amekutana na kufanya mazungumzo na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kuzungumzia mikakati mbalimbali kuelekea msimu wa 2025/26.

Kupitia Instagram akaunti yake Mo ameandika “Tulia. Tathmini. Panga upya.”

Nimefurahi kuwa na mazungumzo ya maana na Kocha Fadlu davids katika msimu wake wa kwanza, akiwa na kikosi kipya na benchi jipya la ufundi, ameiongoza Simba SC kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Chini ya Kocha Fadlu Davids, Simba imefika fainali ya CAF Confederation Cup, fainali ya pili ya kimataifa katika historia ya klabu.

Msimu huu ulikuwa wa kujenga timu. Na bado tukafika fainali, licha ya upinzani mkali.

Simba haitazuilika msimu ujao 🦁💪🏽

#Simba #Nguvumoja 

#LionHeart #SitaachaKuipiganiaSimba

Hakuna maoni: