Breaking

Jumatano, 16 Julai 2025

DKT. NCHEMBA AMEFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA KAMPUNI YA MINARA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya Minara Tanzania, ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo, Bw. Richard Cane, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika kukuza Sekta ya Mawasiliano nchini.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Minara anayesimamia nchi za Afrika na Asia, Bw. Nicholous Vane, pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Kampuni ya Minara Tanzania.




Hakuna maoni: