WIZARA ya Maji kwa kushirikiana na Taasisi ya Chemba ya migodi Tanzania inatarajia kufanya mkutano wa mwaka wa usalama wa mabwawa Novemba 19-21, mwaka huu, Jijini Mwanza.
Mafunzo hayo yatajumuisha wataalam waliobobea kutoka mataifa yaliyoendelea kwenye eneo linalohusu usalama wa mabwawa.
Akizungumza Julai 16,2025,na waandishi wa habari jijini Dodoma , Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Diana Kimario ambaye ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, amesema mafunzo hayo ya tahadhari za dharura za kukabiliana na majanga ni muhimu sana.
“Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeshuhudia majanga yatokanayo na mabwawa ya maji na tope sumu yanapobomoka, hili si jambo geni kwani pia limekuwa likiripotiwa na vyombo vya habari katika nchi za wenzetu ambao wamekumbwa na majanga makubwa zaidi yatokanayo na kubomoka kwa mabwawa hususan ya tope sumu,”amesema.
Amewaalika wataalam na wamiliki wa mabwawa , taasisi na watu binafsi wanaojishughulisha na mabwawa pamoja na wale wanaoishi maeneo yanayozunguka mabwawa kujisajili kwenye mafunzo hayo.
Mkutano huo umeandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni ya City Engineering imekuwa ikiandaa sambamba na mafunzo ya usalama wa mabwawa ya maji na tope sumu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni