Breaking


Jumapili, 24 Agosti 2025

BENKI YA NMB YADHAMINI KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA


Benki ya NMB imedhamini na kushiriki kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichofanyika jijini Arusha, kikiwa na kaulimbiu:

“Ushirikiano endelevu wa Biashara katika Mazingira ya Ushindani wa Kimataifa – Nafasi ya Mashirika ya Umma.”


Kikao hicho kimefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, ambapo viongozi na wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi walihudhuria.


Uwakilishi wa Benki ya NMB umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, CPA. David Carol Nchimbi, pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Juma Kimori. Udhihirisho huu unaonesha dhamira ya NMB kuendelea kushirikiana na mashirika ya umma katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.


#NMBKaribuYako


Hakuna maoni: