Chama Cha Mapinduzi kesho kinatarajia kufanya Harambee kubwa ya kitaifa ya kuchangisha shilingi Bilioni-100 za kusaidia kampeni za chama hicho za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu
Harambee hiyo ya kitaifa itakayofanyika kesho jioni katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es salaam, imetangazwa leo na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dokta Emmanuel Nchimbi katika mkutano wake na Wahariri wa Habari.
Balozi Dokta Nchimbi, ambaye pia ni Mgombea Mwenza wa CCM, amesema, mgeni rasmi katika Harambee hiyo atakua Mwenyekiti wa CCM, Rais Dokta Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa takwimu za CCM, hadi sasa chama hicho kina zaidi ya wanachama Milioni-13 wamesajiliwa kidigitali na kwamba harambe hiyo iko wazi hata kwa vyama vingine vya siasa kuchangia.
Kuhusu chama kupokea fedha kutoka kwa nje ya nchi, Balozi Dokta Nchimbi, amesema chama hicho kitakuwa makini katika kupokea michango ya fedha na hakipo tayari kupokea fedha haramu.
Hapa Chama Cha Mapinduzi kinatangaza akaunti za benki na namba za simu zitakazopokea michango hiyo.
Kampeni za Uchaguzi Mkuu zinatarajiwa kuanza Agosti 28 mwaka huu na kumalizika Oktoba 28 mwaka huu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni