Hii inakuwa mara ya tano kwa mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu, Sean John Combs, anayefahamika pia kwa majina ya kisanii kama Diddy, P. Diddy, na Puff Daddy, kukataliwa kuachiwa huru kutoka katika gereza hatari zaidi jijini New York, linalojulikana kama Metropolitan Detention Center lililoko Brooklyn.
Combs amekuwa akishikiliwa katika gereza hilo tangu Septemba 2024, akihusishwa na kesi nzito zinazomkabili, huku maombi yake ya dhamana yakikataliwa mara kwa mara na mahakama.
Kukwama kwa maombi haya ya dhamana kunazidi kuzua mjadala mpana mitandaoni na katika vyombo vya habari, huku baadhi ya wafuasi wake wakieleza masikitiko yao na kuhoji uhalali wa mchakato wa kisheria unaoendelea.
Kwa sasa, bado haijafahamika ni lini au kama atapewa nafasi nyingine ya kuomba dhamana. Tutaendelea kufuatilia maendeleo ya kesi hii kwa ukaribu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni