Shirikisho la Wachimbaji wa Madini Tanzania-FEMATA linatarajia kufanya kongamano Jumamosi katika mgodi wa Sekenke One, wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Katibu Mkuu wa FEMATA, Rogers Sezero, amesema kongamano hilo litawakutanisha wadau mbalimbali kujadili changamoto, maendeleo na njia bora za kuendeleza sekta ya uchimbaji wa madini.
Sezero, amesema hayo akiwa katika ofisi za madini Mkoa wa Singida, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano hilo.
Aidha, wachimbaji wameishukuru serikali kwa kuruhusu uuzaji wa madini Benki Kuu ya Tanzania-BoT na kuwapatia vifaa vinavyorahisisha kazi kitaalamu zaidi.
Kwa upande mwingine, wachimbaji wanawake wamepongeza serikali kwa kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Wachimbaji Wanawake na kujenga viwanda vya kuchenjua madini ghafi ndani ya nchi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni