Baada ya kufanya usajili wa wachezaji kadhaa sasa ni mwendo wa kuanza kuacha mchezaji mmoja baada ya mwingine. Rasmi sasa klabu ya Azam Fc imetangaza kuachana na golikipa wao namba moja msimu uliopita Mohamed Mustafa ambaye ni raia wa Sudan.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Azam FC mwaka 2023 kwa mkopo kutokea Al Merriekh ya nchini kwao kabla ya kusajiliwa moja kwa moja mwaka jana 2024 kutoka Al Ahl Club of Atbara ambapo huko pia alikuwa kwa mkopo.
Baada ya Mohamed Mustafa kupewa asante ndani ya viunga vya Chamazi kwa wanalambalamba Azam Fc ,ni mchezaji gani atakuwa anafuata kwakupewa naye Thank you baada nyanda Mustafa safari kumkuta?
#Anoldmathias255✍🏾

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni