Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, awamewataki heri watanzania wote katika kuadhimisha sikukuu ya nane nane iliyofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
Leo tunapoadhimisha Sikukuu ya Nanenane, tuna kila sababu ya kujipongeza kwa hatua kubwa ambazo tumepiga kwenye sekta za kilimo, mifugo na uvuvi. Kwa upekee, mwaka huu tumeweka rekodi nyingine ambapo nimezindua Maabara Kuu ya Kilimo, Dodoma, ambayo itatuhakikishia usalama wa chakula tunachokula na tunachouza nje, hivyo kuvutia wanunuzi zaidi.
Serikali yenu imechukua hatua mbalimbali kukuza sekta hizi ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa mitaji, masoko, ruzuku, na kukuza matumizi ya mbolea na mbegu bora. Tumefanya haya tukitambua tija kwenye sekta hizi, ndiyo tija kwa Taifa.
Ninawasihi wananchi kutumia maarifa, hasa ya matumizi ya teknolojia na mbinu bora za uzalishaji waliyoyapata katika Maonesho ya Nanenane kuongeza tija kwenye shughuli zenu.
Pia, kama kaulimbiu ya maonesho haya inavyosisitiza, tujiandae kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya sekta hizi.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni