Breaking


Jumamosi, 30 Agosti 2025

KWA HILI WANA MVOMERO HATUTAKUSAHAU- SARAH

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mvomero,Sarah Msafiri amesema amemshukuru Mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM,),Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kumaliza mgogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji kupitia falsafa yake ya 4R.

Sarah ametoa pongezi hizo Agosti 30,2025,katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais uliofanyika Wami Sokoine,ambapo amesema Mvomero kulikuwa na migogoro mingi hadi kufikia kushindwa kuzikana na kuamua kuchimba mitaro ili kuwatenganisha.

Kupitia maono ya Rais Samia  kwa kushirikiana na viongozi wa dini na kimila kupitia programu ya 'tutunzane' wameweza kuimaliza.

Amefafanua miradi iliyotekelezwa ndani ya miaka minne ya uongozi wa Dokta Samia amesema kulikuwa na miradi 13 ya umwagiliaji  lakini kwa sasa miradi mipya ipo 730 ikiwemo katika Jimbo la Mvomero.

Kutokana na mafanikio hayo amesema wananchi wana kila sababu ya kutiki Okoba 29 mwaka huu  na kumpa kura za kishindo

Hakuna maoni: