Breaking


Jumatano, 27 Agosti 2025

MAPOKEZI YA KATIBU MKUU MPYA WA CCM DKT. ASHA-ROSE MIGIRO

 

Akizungumza wakati Wa Mapokezi yake, Katibu Mkuu mpya wa CCM Taifa, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro,

amemshukuru Mwenyekiti wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na chama kwa ujumla kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kukitumikia chama hicho katika nafasi ya Katibu Mkuu. Uteuzi huo umeweka historia mpya ndani ya CCM kwani kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwake, chama hicho kimepata mwanamke kushika nafasi hiyo ya juu ya utendaji.

Dkt. Migiro pia amemshukuru mtangulizi wake, Balozi Dkt.Emmanuel

Nchimbi, kwa kuweka msingi imara atakaoutumia kama

njia ya kupita katika kutekeleza majukumu yake.

Ameahidi kushirikiana na wazee wa chama na wafanyakazi wote 

katika kipindi hiki cha uchaguzi 

kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo.





#kazinaututunasongambele

Hakuna maoni: