Breaking

Alhamisi, 30 Aprili 2026

RAIS SAMIA ATAMBULIWA KUWA KINARA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA AFRIKA

Umoja wa Afrika kupitia African Union umetambua juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika na kimataifa. Kutokana na mchango huo, amependekezwa kutangazwa rasmi kuwa kinara wa ajenda ya nishati safi ya kupikia Afrika.

Mapendekezo hayo yalitolewa katika Mkutano wa 5 wa Mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanaoshughulikia sekta za nishati na uchukuzi, uliofanyika jijini Johannesburg, South Africa, tarehe 30 Aprili 2026. Katika mkutano huo, Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, aliyeongoza ujumbe wa kitaifa katika ngazi ya mawaziri.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia ametambuliwa kutokana na mchango wake mkubwa katika kusukuma sera, mikakati na ushirikiano wa kimataifa unaolenga kupanua upatikanaji wa nishati safi ya kupikia. Hatua hizi zimeelezwa kusaidia kupunguza athari za kiafya na kimazingira, pamoja na kuboresha maisha ya wananchi, hasa wanawake na watoto.

Akizungumza katika mjadala wa Programu ya Nishati Safi ya Kupikia Afrika, Waziri Ndejembi alieleza kuwa mafanikio ya Tanzania yametokana na uongozi thabiti wa Rais Samia, ambaye ameifanya ajenda hiyo kuwa kipaumbele cha kitaifa. Aidha, alibainisha kuwa nishati safi ya kupikia sasa imejumuishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kama sehemu ya mkakati wa kukuza ustawi wa kijamii na uchumi.

Katika ngazi ya kimataifa, Rais Samia ameendelea kuhamasisha umuhimu wa ajenda ya nishati safi ya kupikia kupitia majukwaa mbalimbali, ikiwemo COP28 na Mkutano wa Nishati Safi ya Kupikia Afrika uliofanyika Paris mwaka 2024. Katika mikutano hiyo, zaidi ya dola za Marekani bilioni 2.2 ziliahidiwa kusaidia utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika.

Hatua ya kumpendekeza Rais Samia kuwa kinara wa ajenda hiyo imeanzia katika ngazi ya wataalamu wa Umoja wa Afrika hadi mawaziri, na sasa inasubiri uthibitisho rasmi katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika, ambapo uamuzi wa mwisho unatarajiwa kutolewa.

Utambuzi huu unaweka Tanzania katika nafasi muhimu ya kuongoza ajenda ya nishati safi ya kupikia barani Afrika, huku ukionyesha dhamira ya nchi katika kulinda mazingira, kuboresha afya za wananchi na kuchochea maendeleo endelevu.

 uliofanyika jijini Johannesburg, South Africa, tarehe 30 Aprili 2026. Katika mkutano huo, Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, aliyeongoza ujumbe wa kitaifa katika ngazi ya mawaziri.

Hakuna maoni: