Breaking

Alhamisi, 14 Agosti 2025

MSANII LAVALAVA ATEMBELEA BASATA, AZUNGUMZA NA DKT. MAPANA KUHUSU MAENDELEO YA SEKTA YA SANAA.

Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Lavalava, leo ametembelea ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kufanya kikao na Katibu Mtendaji, Dkt. Kedmon Mapana, kujadili maendeleo na mustakabali wa sekta ya sanaa nchini.

Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zimejadili nafasi ya wasanii katika kukuza uchumi wa sanaa, changamoto zinazokabili tasnia, pamoja na fursa mpya za ubunifu na ushirikiano wa kimataifa. Dkt. Mapana amempongeza Lavalava kwa mchango wake mkubwa katika kuitangaza Tanzania kupitia muziki, huku akisisitiza umuhimu wa wasanii kushirikiana na BASATA katika kuimarisha ubora na maadili ya kazi za sanaa.

Kwa upande wake, Lavalava ameonesha utayari wa kushirikiana na BASATA katika miradi ya kuibua na kulea vipaji vipya, sambamba na kuhamasisha vijana kutumia sanaa kama ajira na chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Ziara hii inadhihirisha mshikamano kati ya BASATA na wasanii, ikilenga kuijenga sekta imara ya sanaa yenye tija kwa wasanii na taifa kwa ujumla.

Hakuna maoni: