Breaking

Alhamisi, 14 Agosti 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI: MAN CITY WANAMUWINDA SIMONS ANAYELENGWA NA CHELSEA

 

Manchester City wanafikiria namna ya kuuteka nyara uhamisho wa Chelsea wa kumnunua winga wa RB Leipzig wa Uholanzi Xavi Simons, 22. (Sport) 

Brighton watahitaji zaidi ya pauni milioni 100 kwa Carlos Baleba baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21. (Telegraph - subscription required) 

Mshambulizi wa Denmark Rasmus Hojlund yuko tayari kuondoka Manchester United msimu huu wa joto huku AC Milan ikijaribu kufanya mazungumzo ya mkataba wa mkopo na chaguo la kununua. (Gazzetta dello Sport - In Italian)


Manchester City wamemuongeza Maghnes Akliouche wa Monaco kwenye orodha ya wanaolengwa na watachuana na Bayer Leverkusen katika kuinasa saini ya winga huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23. (Florian Plettenberg)

#ChanzoBbcswahili


Hakuna maoni: