Arusha:Benki ya NMB Yatambuliwa kwa Mchango Wake Katika Kikao Kazi cha Viongozi wa Taasisi za Umma.
Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kimehitimishwa rasmi jijini Arusha na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.
Katika hafla ya kufunga kikao hicho, Benki ya NMB ilitunukiwa cheti maalum cha kutambua mchango na nafasi yake katika kufanikisha mkutano huo muhimu uliowakutanisha viongozi wakuu kutoka taasisi mbalimbali za umma nchini.
Cheti hicho kilipokelewa kwa niaba ya benki na Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Bw. Baraka Ladislaus.
Tuzo hiyo ni kielelezo cha namna NMB inavyoshirikiana na wadau wa sekta ya umma katika kuunga mkono juhudi za kitaifa za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
#NMBKaribuYako




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni