Breaking


Jumapili, 10 Agosti 2025

SERIKALI KUENZI MCHANGO WA HAYATI NDUGAI-RAIS DK SAMIA.

          Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta SAMIA SULUHU HASSAN, leo amewaongoza Waombolezaji kuuaga Mwili wa aliyekua Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati JOB NDUGAI.

Shughuli hiyo imefanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya Siasa na wananchi.

          Akizungumza katika shughuli hiyo, Rais Dokta SAMIA amesema Hayati NDUGAI aliaminiwa ndani ya Taifa la Tanzania na nje ya Tanzania.

          Pia amesema Hayati NDUGAI alikua mkomavu wa Kisiasa na Kiuongozi na Taifa litamkumbuka kama Mwanasiasa aliyependa na kuthamini Maendeleo ya Vijana ikiwemo Elimu kwa watoto wa Kike.

          Rais Dokta SAMIA amewaeleza waombolezaji kwamba Serikali itaenzi mchango alioutoa Hayati NDUGAI kwa Taifa kwenye nyanja mbalimbali.

          AWALI Spika wa Bunge Dokta TULIA ACKSON, amesema Hayati NDUGAI alisimamia mageuzi ya kiutendaji katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alikua Mwalimu mwema na mwalimu wa nidhamu.

          Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara STEPHEN WASIRA, amesema Mchango wa Hayati NDUGAI ni mkubwa katika Taifa la Tanzania.

          Pia amesema CCM inautambua mchango wa Hayati NDUGAI kwa Nchi.

          Mwili wa Hayati NDUGAI utazikwa kesho Kijijini kwake Sejeli katika Kata ya Sejeli wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.



Hakuna maoni: