Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa amesema kuwa, Serikali imenunua tiketi 10000 zenye thamani ya shilingi Milioni 20, kwa ajili ya mashabiki kuingia uwanjani kuishangilia Taifa Stars katika mchezo wake dhidi ya Madagascar mchezo utakaochezwa leo Agosti 9, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Msigwa amesema hayo, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, na kusisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia Taifa Stars ili iendelee kufanya vizuri katika michuano ya CHAN 2024 inayoendelea nchini Tanzania, Kenya na Uganda.
Tiketi hizo watafaidika nazo mashabiki elfu 10 watakaowahi kuja kuanzia saa nane na zitapatikana katika mageti yote kwa 'Volunteers' na atayekosa asinunue tiketi za watu wanaoshika . mkononi isipokuwa katika magari ya N Card.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni