Breaking


Jumatano, 20 Agosti 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO: ASTON VILLA SASA YAVUTIWA NA NICOLAS JACKSON WA CHELSEA

 

Aston Villa inachunguza uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, kutoka Chelsea lakini bei inayotakiwa inapaswa kuwa chini ya £60m kutokana na vikwazo vya kifedha vya klabu hiyo ya West Midlands. (Telegraph - Subscription)

Uhamisho wa Bayern Munich kumnunua fowadi Mfaransa Christopher Nkunku, 27, umekwama, na hivyo kuchelewesha majaribio ya Chelsea kumsajili kiungo wa kati wa RB Leipzig na Uholanzi Xavi Simons, 22. (Guardian)

Chelsea wanatazamia kuongeza juhudi zao za kumsajili fowadi wa Argentina Alejandro Garnacho kutoka Manchester United lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 hataruhusiwa kuondoka Old Trafford kwa bei nafuu. (Evening Standard)

Newcastle haiko tayari kulipa zaidi ya pauni milioni 40 kumnunua mshambuliaji wa Brentford Yoane Wissa lakini The Bees wameweka bei ya pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa DR Congo mwenye umri wa miaka 28. (Northern Echo )


Mshambulizi wa Wolves Jorgen Strand Larsen bado anavutiwa na Newcastle - ingawa Mnorwey huyo mwenye umri wa miaka 25 hana mpango wa kuondoka Molineux. (The Athletic - Subscription)


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: