Breaking


Jumatatu, 11 Agosti 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU: GREALISH AKUBALI KUJIUNGA EVERTON KWA MKOPO

 

Winga wa Uingereza Jack Grealish, 29, amekubali kujiunga na Everton kwa mkopo kutoka Manchester City . (TeamTalk) 

Chelsea wanafanya mazungumzo na RB Leipzig kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Xavi Simons, 22, jambo linaloweza kumaanisha kuwa mshambuliajii wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, atarejea katika klabu hiyo ya Ujerumani. (Guardian) 

Nicolas Jackson anapendelea kuhamia Newcastle United iwapo mshambuliaji huyo wa Senegal, 24, ataondoka Chelsea wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Telegraph -subscription required)n


Newcastle wamewasilisha ombi la kumnunua Yoane Wissa wa Brentford lakini Liverpool wanafuatilia hali hiyo huku wakimuona mshambuliaji huyo wa DRC , 28, kama kiungo mbadala wake iwapo watashindwa kumsajili Isak. (Caught Offside) 

Newcastle itasubiri kusuluhisha mustakabali wa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, kabla ya kuamua kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Jackson. (Shirika la habari la PA), nje



Hakuna maoni: