Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) amesema Sheria ya fedha ya mwaka 2025 imefuta jukumu kwa TRA la kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo na sasa jukumu hilo limehamishiwa Mamlaka nyingine kama vile Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalumu na badala yake Sheria imeweka jukumu kwa TRA kwa kushirikiana na Mamlaka hizo kuwatambua na kuwapa TIN wajasiriamali hao.
Ameyasema hayo tarehe 15.08.2025 katika Semina ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa wafanyabiashara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyofanyika katika katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
CPA. Walalaze amefafanua kuwa wafanyabiashara wadogo ambao mauzo ghafi yao kwa mwaka yatafikia Shilingi Milioni 4, wataanza kulipa kodi ya mapato.
Ameongezea kuwa Sheria hiyo pia imeelezea kuwa Waziri mhusika atatoa kanuni za jinsi kuwasimamia wajasiriamali hao.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni