Kwa mwaka wa pili mfululizo, Benki ya NMB imeendelea kuwa mdhamini mkuu wa Tamasha la Kariakoo Festival, lenye lengo la kuwainua wafanyabiashara wadogo, kati na wakubwa kupitia suluhu bunifu za kifedha.
Uzinduzi huu umefanyika mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Suleiman Jaffo, aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa serikali. Uongozi wa Benki umeongozwa na Mkuu wa Idara ya Biashara, Bw. Alex Mgeni aliyeongozana na viongozi wengine wa Benki.
Wafanyabiashara na wananchi wanakaribishwa sana kwenye banda letu ili kupata huduma zote za kibenki na elimu ya fedha.







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni