Katibu wa kamati, Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ( NEC ) ya Chama Cha Mapinduzi , Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar Hamis Mbeto amewataka wananchi kukichagua Chama Cha Mapinduzi.
Mbeto, ameyasema haya visiwani Zanzibar katika uzinduzi wa Kampeni za Uchagu wa Jimbo la wakati wa kuwaombea kura wagombea wa CCM kupitia nafasi ya Ubunge wa Jimbo, Uwakilishi na Udiwani.
Mbeto, amesema Wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wanajivunia serikali ya awamu ya nane, Chini ya Dokta Hussein Ali Mwinyi, mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM kwa kipindi cha pili, imefanya mambo mengi ,miradi mingi ambayo inaonekana lakini Hamza yeye ndio muendeshaji wa miradi yote.
Amebainisha kuwa atashangaa sana kama kutatokea kura hata Moja kuwapugia vyama pinzani, wakati Mgombe wa Hamza amefanya kazi nzuri , na ameoata nafasi ya kuendelea kufanya kazi nzuri na ndio maana wananchi wa shauri moyo wamekuchagua tena ili tuendelee kuwatumikia tena.
Mbeto amewaomba wananchi kumchagua mbunge Mattar kwa kumpa sifa za Jembe na amini sisi
tunaocheza mpira wa miguu tunatumia mfumo wa 4 Kwa mbili ni mfumo wa kupata ushindi.
Kwa muda mchache yaliyofanywa ni Makubwa hivyo siku ya kupiga kura wagombea wa CCM tuwape kura wote na kuwachagua Kwa kura nyingi sana kwa kujua ilani mpya CCM ni maendeleo nje hadi ndani.
Amesema kwenye ilani ya chama Cha mapinduzi ya mwaka 2020 hadi 2025 kwenye sekta ya elimu ilimuagiza Dokta Hussein Ali Mwinyi kujenga madarasa 1500 lakini kajenga madarasa 5000 , na shule 10 za ghorifa 3 lakini amejenga shule 60.
Aidha, amewataka wanachama hamasa iliyopo katika mikutano mwaka huu, ndiyo itumike kwa kila mwana ccm ahakikishe akapige kura na sio kushiriki tu kwenye kampeni peke yake.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni