Breaking

Jumatano, 24 Septemba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA: CRYSTAL PALACE HAINA NIA YA KUMUUZA WHARTON

 

Crystal Palace imeiambia Liverpool kuwa haina nia ya kumuuza kiungo wa kati wa England Adam Wharton, 21, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Team talk)

Liverpool inajiandaa kumpa kiungo wa kati wa Uholanzi Ryan Gravenberch, 23, mkataba mpya wa muda mrefu. (Team talk)

Arsenal ina nia ya kumsajili winga wa Japan Takefusa Kubo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Real Sociedad wakati wa uhamishowa wa wachezaji mwezi Januari mwakani. (Fichajes - kwa Kihispania)

#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: