Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania - JWTZ limemshukuru Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulitengeneza na kuliwezesha Jeshi kutekeleza majukumu yake kikamilifu ikiwemo ya michezo.
Shukrani hizo zimetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda katika hafla Maalumu ya kumpongeza Sajinitaji Alphonce Simbu kwa kushinda medali ya dhahabu huko Tokyo Nchini Marekani, hafla iliyoenda sambamba na kuzipongeza timu nyingine za majeshi ikiwemo Timu ya Mpira ya Miguu ya Wanawake JKT Queens.
Jenerali Mkunda amesema mchango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni wa thamani kubwa na ndio unaowawezesha kufurahia mafanikio makubwa ya kimichezo Jeshini.
Aidha amewapongeza wanamichezo wote walioibuka washindi katika mashindano mbalimbali pamoja na wasimamizi wao wa karibu ambao wamewasaidia katika ushindi huo.
Kwa kutambua umuhimu wa Michezo Jeshini, Jenerali Mkunda amesema Makao Makuu ya Jeshi itaendelea kutoa kipaumbele na kukuza vipaji na kuhakikisha wanamichezo wa Jeshi wanapata mazingira mazuri ya kufanikisha malengo yao.
Aidha ametoa wito kwa wanamichezo wengine Jeshi kuendelea Kupambana na kujituma kwa nidhamu ili wawe wanamichezo Bora kwa kuwa michezo ni sehemu ya kazi ya Jeshi.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni