Breaking


Jumatano, 17 Septemba 2025

JWTZ YAWATAKA WANAJESHI WAKE KUIWAKILISHA VYEMA TANZANIA KATIKA OPERESHENI YA AMANI LEBANON

 Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania-JWTZ- limewasisitiza wananjeshi wake kuishi kwa viapo vyao ikiwa ni pamoja na kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania na ya Umoja wa Mataifa wanapotekeleza majukumu ya Ulinzi wa Amani.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi Tanzani Brigedia Jenerali GEOGRE ITANG’ARE, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ- Luteni Jenerali OTHMAN OTHMAN, katika zoezi la kukabidhi bendera ya Tanzania kwa Kikosi kinachokwenda kushiriki Ulinzi wa Amani nchini Lebenoni.

 Brigedia Jenerali ITANG’ARE, amesema kikundi hicho ambacho kinaundwa na Kombania mbili za Polisi Jeshi kitakwenda kuhudumia nchini Lebanoni kwa Kipindi cha mwaka mmoja huku kikiwa na watu 125.

Amesema umoja wa mataifa umekuwa na Imani kubwa na kikundi cha polisi jeshi tangu mwaka 2007 kilipoanza kuhudumia nchini Lebanon na hakujawahi kutokea utovu wa nidhanu na ndio sababu ya Umoja wa Mataifa kuongeza ushiriki wa Tanzania katika ulinzi wa amani kwenye maeneo mengine.

 Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi kinachoenda kushiriki Ulinzi wa Amani Luten Kanal ABDALLAH HUSSEIN RAJAB, amesema kulingana na maelekezo ya Makao Makuu ya Jeshi wamejipanga kwenda kutekeleza majukumu ya Umoja wa Mataifa kulingana na Azimiao lililoanzisha Oparesheni ya Lebanon.

Naye Kaptain FATUMA JUMA ADAM, Mwakilishi wa kikundi hicho kinachokwenda kutekeleza jukumu la Umoja wa Mataifa la Ulinzi wa Amani nchini Lebanon amesema wao kama wanawake wamejipanga kutekeleza majukumu yote ambayo yameainishwa na Jeshi na umoja wa mataifa.

Hakuna maoni: