Breaking

Jumatatu, 22 Septemba 2025

MAJIKO BANIFU TEKNOLOJIA YA KISASA INAYOTUMIA MKAA KIDOGO

Imeelezwa kuwa majiko banifu yanayotolewa kwa bei ya ruzuku na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni majiko yanayotumia kiasi kidogo cha mkaa kulinganisha na majiko mengine ya mkaa. 

Hayo yamebainishwa na Wataalam kutoka REA wanaoendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita. 

Aidha, majiko banifu yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kupunguza sumu ya mkaa (carbon monoxide) hivyo inasaidia kupunguza madhara ya kiafya yatokanayo na nishati ya mkaa. 

Halikadhalika, majiko banifu yanasaidia utunzaji wa mazingira, ni rahisi kwa matumizi yanadumu kwa muda mrefu bila kupata changamoto ya kuharibika kwa watumiaji. 

Katika mkoa wa Geita kampuni inayosambaza majiko banifu kwa bei ya ruzuku ni Geita Millenium Star Company Limited.

Hakuna maoni: