Breaking


Jumatatu, 22 Septemba 2025

OCTOBA, 29,TUTAOTA MOTO NA WEWE MPAKA KIELEWEKE- JENISTA

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma,Jenista Mhagama,amesema miundombinu ya afya iliyoweka na serikali ya awamu ya sita chini ya  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,imesaidia kupunguza vifo vya wanawake wanaojifungua kutoka 556 mpaka 114 kwa kila kundi la wanawake 100,000 kwa Jimbo la Peramiho.

Jenista amesema hayo Septemba 22,2025,wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais Dkt.Samia,unaofanyika katika uwanja wa VETA,Songea Mjini 

"Tumejengewa hospitali za wilaya kwenye halmashauri zetu,vituo vya afya  zahanati vimewekewa vyumba maalum vya uzazi wa dharura, matokeo yake tumepunguza vifo vitokanavyo na uzazi,sisi wanawake bila ya kujali itikadi zetu tunakushukuru sana kwa kujali afya zetu na tunasema Octoba tunatiki,"amesema.

Amemshukuru pia kwa utoaji wa ruzuku ya Pembejeo iliyoleta matokeo makubwa kwa wana Ruvuma ikiwemo kuongeza uzalishaji kutoka tani Milioni 1.3 hadi Milioni 1.5,na hivyo kuwezesha upatikanaji wa mabati kwa wananchi 

Hakuna maoni: