Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza zoezi la elimu ya kodi mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke mkoani Dar es salaam kwa lengo la kutoa elimu, kusikiliza changamoto na kuwakumbusha wafanyabiashara kufanya malipo ya awamu ya tatu kwa wakati.
Zoezi hilo lililoanza Jumaatatu wiki hii, limezindiliwa rasmi jana tarehe 09.09.2025 na Meneja wa TRA mkoa wa Kikodi Temeke, Bw. Masau Malima ambae pia alishiriki kutoa elimu ya kodi na kuwasikiliza wafanyabiashara wa Keko wilaya ya Temeke.
Akizungumzia zoezi hilo, Bw. Malima amsema lengo la zoezi hilo ni kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya mambo mbalimbali ya kodi, kusikiliza changamoto zao, kuchukua maoni yao kwa lengo la kuboresha huduma za TRA na kuwakumbusha kulipa kodi awamu ya tatu kabla au mnamo tarehe 30.09.2025 ili kuiwezesha serikali kukamilisha miradi ya maendeleo na kijamii kwa wakati.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni