Breaking

Jumamosi, 6 Desemba 2025

KMC YAACHANA NA KOCHA WAKE MAXIMO

 


Klabu ya KMC imethibitisha kuachana rasmi na Kocha Mkuu, Stewart Hall Maximo, baada ya makubaliano ya pande zote mbili. Uongozi wa klabu hiyo umesema uamuzi huo umefikiwa kwa nia ya kuboresha mwenendo na matokeo ya timu katika ligi.


Katika taarifa yao, KMC imeeleza kuwa inamshukuru Maximo kwa mchango wake katika kipindi alichoiongoza timu na inamtakia mafanikio mema katika majukumu yake yajayo. Aidha, mchakato wa kusaka kocha mpya umeanza ili kuhakikisha timu inaendelea kuwa kwenye ushindani.


KMC imewahakikishia mashabiki kuwa itaendelea kufanya maboresho muhimu kwa ajili ya mafanikio ya muda mrefu ya klabu.


#Official-Isharoja✍🏾✍🏾✍🏾


Hakuna maoni: