WANANCHI wa Iramba Mkoani Singida,wapo tayari kumlaki na kumsikiliza mgombea wa Urais kupitia
Chama Cha Mapunduzi(CCM),Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,akinadi
sera na Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho 2025-2030.
Rais Samia anafanya Mkutano Iramba katika viwanja vya Lulumba Septemba 10,2025,baada ya jana Septemba 9,2025,kufanya mikutano Manyoni,Ikungi na Singida Mjini.
Baadhi ya mambo aliyoyaahidi wakati akihutubia mikutano hiyo ya kampeni ni ujenzi wa vituo vya afya,Kongani za viwanda,ghala la kuhifadhia chakula,vituo vya ukodishani wa zana za kilimo,maji na miundombinu ya barabara.
Baada ya kumaliza mkutano huo,Rais Samia ataelekea Mkoa wa Tabora ambapo atafanya mkutano Igunga na Nzega Mjini.









Hakuna maoni:
Chapisha Maoni