Breaking

Jumatano, 24 Septemba 2025

MSIGWA ATEMBELEA KAMBI YA SIMBA NA KUKABIDHI GOLI LA MAMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali  Ndg. Gerson Msigwa Septemba 23, 2025 ameitembelea  timu ya simbasctanzania Bunju jijini Dar es salaam, kwa lengo la kukabidhi kiasi cha shilingi Milioni tano zawadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa timu hiyo, mara baada  ushindi walioupata ugenini dhidi ya timu ya Gaborone United ya nchini Botswana.



Akipokea zawadi hiyo, Nahodha wa Simba Shomari Kapombe, alisema  wanashukuru kwa hamasa hiyo na wameahidi kufanya vizuri  zaidi kwenye mchezo wa marudiano tarehe 29 Septemba, 2025 Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.


#Official-Isharoja ✍🏾

Hakuna maoni: