Breaking


Ijumaa, 12 Septemba 2025

TBA KUANZA OPARESHENI YA KUWATOA WADAIWA SUGU

 

WAKALA wa majengo Tanzania-TBA umewataka  wapangaji WA nyumba za kuishi , za biashara na walipanga kwenye maeneo ya wakala huo ambao wanamadeni ya Kodi ya na malimbikizo ya nyuma kulipa madeni hayo mpaka kufikia September 30 Mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mtendaji wa TBA, Architec Daud Nkondoro ambapo amesema Hadi Sasa jumla ya deni la pango za nyumba za TBA ni Zaidi ya Bilioni 4.5 na deni Hilo limetokana na uwepo WA wadaiwa sugu ambao hawajalipa Kodi za pango Katika kipindi Cha miezi mitatu na kuendelea.

Ameeleza kuwa wadaiwa ambao hawatalipa madeni Yao ndani ya muda uliotolewa wataondolewa kwenye nyumba za wakala au maeneo waliyopangishwa pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.


Kwa upande wake Mkurugenzi WA milki kutoka TBA, FRV Said Mndeme amebainisha kwamba   zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu litaanza rasmi October mosi Mwaka huu huku akibainisha kuwa asilimia kubwa ya madeni ya pango yapo Katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Aidha TBA imesema inaendelea na ujenzi wa nyumba za kupandisha watumishi WA umma Katika maeneo mbalimbali nchini.

Hakuna maoni: