Real Madrid wanafuatilia kandarasi ya mlinzi wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, kwa nia ya kumsajili kama mchezaji huru msimu ujao mkataba wake wa sasa utakapokamilika. (ESPN)
Beki wa Uingereza John Stones, 31, anatazamiwa kuanza mazungumzo na Manchester City kuhusu mkataba mpya na mkataba wake wa sasa unaotarajiwa kumalizika msimu wa joto. (Mirror)
Aston Villa wanafikiria kutoa ofa kwa mshambuliaji wa Sunderland mwenye umri wa miaka 25 Wilson Isidor mwezi Januari. (Football Insider)
#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni