Breaking


Jumapili, 28 Septemba 2025

TFS YAZIDI KUNG’ARA KWENYE SEKTA YA UFIGAJI NYUKI – MAONESHO YA MADINI GEITA 2025

Katika kilele cha Maonesho ya Madini Geita leo, Septemba 28, 2025, banda la TFS kupitia Shamba la Miti Silayo limekuwa kivutio kikubwa kwa wageni na wadau wa maendeleo ya maliasili.

TFS imeonesha kwa vitendo namna misitu ya hifadhi inavyoweza kuwa chanzo cha uchumi jumuishi, kwa kuibua fursa nyingi kupitia sekta ya nyuki. Wageni waliweza kushuhudia:

 *Bidhaa bora*: Asali safi na nta ya asili, bidhaa zinazotambulika kitaifa na kimataifa kwa ubora wake.

 *Vifaa vya kisasa*: Mizinga ya nyuki yenye uhai, mavazi ya uvunaji salama, kifaa cha kukamulia asali, na teknolojia nyingine zinazoboresha tija na usalama kwa wafugaji nyuki.

 *Ushuhuda wa uhalisia*: Wageni walipata fursa ya kuona nyuki hai na kujifunza hatua kwa hatua safari ya asali kutoka mzinga hadi mezani.

Kupitia ushiriki huu, TFS imeweka wazi dhamira yake ya kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki kwa faida ya jamii na Taifa, huku ikihakikisha huduma zote za nyuki na misitu zinapatikana kwa urahisi kupitia ofisi zake katika kila wilaya Tanzania Bara, mashamba, pamoja na njia za kidigitali.


*_Misitu ni Utajiri – Asali ni Afya, Uchumi na Fursa kwa Kila Mtanzania_*.

Hakuna maoni: