Breaking

Jumamosi, 20 Septemba 2025

TUSIKUBALI KUCHOKOZEKA-RAIS SAMIA.

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan,amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wamejitahidi kusimamia utulivu wa kisiasa,usalama na amani hivyo kuwaomba wananchi kutokubali kuchokozeka.


Rais Dkt. Samia ametoa ombi hilo Septemba 20,2025,wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Gombani ya Kale Pemba.


"Kipindi hiki watu wengine wanakitumia kuchokozana,niwaombe msikubali kuchokozeka,kuweni kama mimi mtoto wenu, mama yenu,dada yenu,shangazi yenu,nachokozwa sana lakini sichokozeki,tusivunje amani iliyopo kwa sababu ya uchaguzi,"amesema.

Hakuna maoni: