Breaking

Ijumaa, 17 Oktoba 2025

MADAKTARI BINGWA WAFANIKIWA KUONDOA JIWE KWENYE KIBOFU CHA MKOJO

Timu ya Madaktari Bingwa imefanikiwa kufanya upasuaji kwa Bw. Ramadhan Bilali, mkazi wa shinyanga mwenye umri wa miaka 55, na kuondoa jiwe kwenye kibofu cha mkojo lililomsumbua kwa  miaka sita bila kupata ufumbuzi.

Akizungumza  Oktoba 16, 2025, Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dkt. Joachim Kisaka, amesema upasuaji huo umefanyika katika hospitali ya Ushetu, mkoani Shinyanga, kupitia Kambi ya Madaktari Bingwa.

Dkt. Kisaka amesema kuwa mgonjwa huyo amekuwa akitafuta tiba katika hospitali mbalimbali kwa gharama kubwa bila mafanikio. Baada ya kufanyiwa upasuaji huo, anaendelea vizuri na hali yake inaimarika kwa kasi.

Aidha, Dkt. Kisaka amebainisha kuwa upasuaji huo ni miongoni mwa huduma muhimu zinazotolewa na madaktari bingwa katika kambi hiyo.

Hakuna maoni: