Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga amefariki akiwa na umri wa miaka 80.
Raila amefariki wakati akifanyiwa matibabu katika hospitali moja nchini India kulingana na duru za familia.
Magazeti ya India Mathrubhumi na The Hinduyaliripoti habari hiyo kwa mara ya kwanza Jumatano asubuhi, yakisema Odinga alipatwa na mshtuko wa moyo wakati wa matembezi ya asubuhi katika Hospitali ya Macho ya Sreedhareeyam Ayurvedic na Kituo cha Utafiti, ambako amekuwa akitibiwa kwa siku tano zilizopita.
Msemaji wa kituo hicho aliiambia AFP kwamba Odinga alipata matatizo ya kupumua na kuzimia mwendo wa saa 07:45 asubuhi. Alikimbizwa katika hospitali ya kibinafsi ya karibu, lakini hali yake ilidhoofika.
#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni