Breaking


Alhamisi, 9 Oktoba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI: FERNANDES ANATAKA KUSALIA MAN UTD

 

Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes ,31, hana mpango wa kuondoka klabu hiyo mwezi Januari licha ya Mreno huyo kumezewa mate na vilabu kadhaa ya Saudi Arabia.(Talksport)

Mlinzi wa kati wa United na timu ya England Harry Maguire ,32, ana imani ya kupewa mkataba mpya baada ya mkataba wake kukamilika mwisho wa msimu huu.(Sun).

Kiungo wa kati wa Manchester City Bernardo Silva,31, anajipanga kufunganya virago aondoke klabu hiyo mwisho wa msimu huu, hata hivyo kuna vilabu kadhaa vya Saudia na pia Benfica ya Ureno wote wanainyemelea saini yake. (Givemesports)


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: