Beki wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 25, amempiku beki wa kati wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, kama mchezaji anayepigiwa upatu kusajiliwa bila malipo na klabu ya Real Madrid msimu ujao. (Fichajes - kwa Kihispania)
Liverpool wanavutiwa na beki wa kati wa Bayern Munich na Ufaransa Dayot Upamecano, 26, pamoja na Guehi wa Crystal Palace. (Florian Plettenberg)
Tottenham ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Brentford Mjerumani Kevin Schade, 23. (Sky Germany via Sky Sports)
Juventus wanamtaka mlinda lango wa AC Milan Mfaransa Mike Maignan, 30, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao. Kipi huyo pia anawaniwa na Chelsea na Bayern Munich. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni